Hamida Hassan na Gladness Mallya
SIKU chache baada ya mama wa marehemu
Steven Kanumba, Flora Mtegoa kukiri
kwamba Elizabeth Michael ‘ Lulu ’ alikuwa
mkwe sahihi kwake , safari hii ameibuka na
kumbariki Wema Sepetu ambaye naye
aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na
mwanaye, akisema ana huruma, roho nzuri
na utu .
Mama Kanumba , Flora Mtegoa.
Akizungumza kwa kujiamini, mama
Kanumba alisema: “ Hili nalizungumza
kutoka moyoni mwangu, huyu mtoto ana
moyo wa upendo sana. Angalia namna
anavyowasaidia wenzake wanapopata
matatizo . Anajitoa kwa moyo , siyo mchoyo .
Kwa kweli Mungu amwongezee .”
Wema Sepetu .
“ Kiukweli Wema anajitoa sana. .. nakumbuka
hata kipindi akiwa na mwanangu , maana
uhusiano wao niliutambua, Kanumba
mwenyewe alinitambulisha ; walikuwa wakija
kunisalimia nyumbani ananiita pembeni na
kunipa pesa ili Kanumba asione, akitaka na
yeye anipe. Huo ni moyo wa kipekee sana, ”
alisema mama huyo .
Hiki ni kama kipindi cha mama huyo
kuonesha hisia zake kwa wakwe zake
(wasichana waliowahi kuwa na uhusiano na
marehemu mwanaye) kwani takribani wiki
tatu zilizopita , alimzungumzia Lulu kwa
maelezo kuwa alikuwa mkwe sahihi kwake.
Thursday, February 13, 2014
MAMA KANUMBA AMBARIKI WEMA
Labels:
news
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment