Monday, February 03, 2014

WEMA:NIKIFA NIAGWE UWANJA WA TAIFA

Kazi ipo ! Beautiful Onyinye, Wema Isaac
Sepetu ambaye huwa haishiwi habari,
ameibuka na jipya akidai kuwa akifa leo au
kesho basi aagwe Uwanja wa Taifa jijini Dar,
Ijumaa Wikienda limemtegea sikio.
Wema Isaac Sepetu .
Miss Tanzania huyo wa 2006 /07 ambaye
anakimbiza kwenye sinema za Kibongo
alifunguka hayo wikiendi iliyopita wakati
akiwa safarini kuelekea jijini Arusha ambapo
msanii anayemilikiwa na kampuni ya Wema
ya Endless Fame Production aliyetajwa kwa
jina moja la Mirrow alikwenda kuangusha
shoo pande hizo .
Wema aliyasema hayo alipokuwa akichangia
mada ya utabiri wa mtoto wa aliyekuwa
mtabiri bingwa , marehemu Sheikh Yahya
Hussein, Maalim Hassan Hussein aliyetabiri
kwamba wasanii wengi wenye majina
makubwa watakufa mwaka 2014 .
Mwanadada huyo alisema mastaa wengi
wameaga dunia na kuagwa kwenye Viwanja
vya Leaders, Kinondoni lakini yeye itakuwa
Uwanja wa Taifa .
Alitolea mifano ya waliokuwa mastaa kama
Steven Kanumba, Albert Mangweha ‘ Ngwea ’ ,
Julius Nyaisangah ‘Anko J ’ na wengine kuwa
waliagwa Leaders lakini kwa namna
ambavyo jina lake ni kubwa ndani na nje ya
Bongo viwanja hivyo havitatosha .
“ Mimi nakwambia kabisa , pale Leaders
hapatatosha . Kama nikifa leo au kesho ,
niagwe Uwanja wa Taifa ili kila mtu apate
nafasi . Naamini watu watakuwa wengi sana
so Leaders hapatatosha , ” alisema staa huyo
mkubwa anayeminya kilamalavidavi na
Mbongo Fleva , Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz ’ .
Ijumaa Wikienda lilipododosa kwa marafiki
zake wa karibu lilitonywa kwamba tayari
jambo hilo alishawaeleza na kwamba
aliomba iwe hivyo.
Mbali na wasanii, Maalim Hassan alitabiri
pia kuwa mwaka huu kuna mwanasiasa
mkubwa atakufa na utakuwa msiba wa
kitaifa, vifo vya wanahabari na malumbano
makubwa juu ya serikali tatu .
Wiki iliyopita ilijaa simanzi baada ya kufariki
dunia kwa watu maarufu kama mchekeshaji
wa Futuhi ya Star TV , Omary Majuto ‘ Mzee
Dude’, mpiga ngoma wa Bendi ya The
African Stars ‘ Twanga Pepeta ’ , Soud
Mohamed ‘ MCD ’ , mwigizaji wa Bongo
Movies , Victor Peter na mtangazaji wa East
Africa Radio, Kenneth Kidago Lyanga.
Jodat King

GP

No comments:

Post a Comment