Sunday, February 16, 2014

ROSE NDAUKA:NUSURA WATOTO WANIVUE NGUO

MWIGIZAJI mahiri Bongo, Rose Ndauka
amefunguka kuwa amenusurika kuvuliwa nguo
na watoto ambao walipandwa na midadi baada
ya kumuona ‘live’.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika sherehe
ya arobaini ya mwanaye iliyofanyika nyumbani
kwao, Tandale-Tanesco, jijini Dar ambapo
watoto hao walimvizia Rose alipotoka nje,
walimvaa na kuanza kumng’ang’ania nguo.
“Hawakutegemea kuniona pale, wengi
wamezoea kuniona kwenye TV. Daah nilipata
wakati mgumu kidogo maana ilibaki kidogo
wanivue nguo, lakini nashukuru Mungu
niliwatuliza, wakanielewa nikarudi zangu
ndani,” alisema Rose

No comments:

Post a Comment