Monday, February 17, 2014

‘DIAMOND HAWEZI KUNIPATA MIMI,ATAWACHEZEA WENGINE‘AMISA

MREMBO anayedaiwa kuliingilia penzi la staa
wa filamu Bongo, Wema Sepetu na Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’, aliyewahi kushiriki
Shindano la Miss Tanzania, Amisa Mabeto
amefunguka kuwa mwanamuziki huyo ni
shemeji yake tu, hakuna chochote kati yao.
Akipiga stori na safu hii kuhusiana na madai
hayo, Amisa alisema alistaajabu kwani hana
mazoea na Diamond Kama ni kuonana waliwahi
kuonana miaka ya nyuma, tena siyo kimapenzi.
“Kamwe siwezi kutembea na Diamond na
haitatokea kwani jamii nzima inajua yupo na
Wema na mimi huyo mtu ni rafiki yangu
mkubwa, hana chake hapa, siwezi kutembea
naye kamwe, namheshimu kama shemeji
yangu,”

No comments:

Post a Comment