Mcheza filamu za kibongo Riyama Ally anaetisha katika filamu za kulia lia amesema licha ya kipaji alichonacho lakini hamfikii msanii mwenzake Wastara Sajuki.
Amemtaja msanii huyo kuwa anauwezo mkubwa wa kuigiza vyovyote inavyoitajika na kwamba ni nadra sana kupata waigizaji wa aina hiyo
Riyama amesema yeye anakubalika kwa kuigiza kulia lakini amewataka wadau waelewe kwamba Wastara ndio analia zaidi na anafanya hivyo kwa kuzingatia uhalisia wa sehemu anayoigiza
“Mimi nalia lakini pamoja na yote namkubali sana Wastara yeye anajua zaidi lazima niseme ukweli?
No comments:
Post a Comment