Wednesday, February 26, 2014

Diamond,Wasanii watumie ujuzi kukuza sanaa kuliko kupiga majungu

Diamond Ni msanii anayefatiliwa
na kuandikwa zaidi kwenye
mitandao kuhusu Muziki na
Maisha yake, Ni msanii mwenye
kazi nzuri na vituko pia kwenye
sanaa ndio maana anajikuta
akiwa na mashabiki wengi
kwenye mambo tofauti
anayofanya.
Leo Diamond ameonekana
kukerwa na mambo ya majungu
kuhusu muziki na maisha yake
na kupitia instagram yake
aliandika hivi.
“kiukweli, nasikitishwa sana jins
baadhi ya wasanii kutwa
wanavyolazimisha
kunitengenezea ugomvi wa
kilazima pasipo kuwa na sababu,
mara wengine wakizusha eti
Nimewatusi kwenye Media, Mara
sjui Nimepost kuwakashif, yaani
ilimradi tu….kwanini Wanamuziki
wa Tanzania Tunashindwa
kubadilika… mbona mi
nahangaika na muziki wangu
kimpango wangu… Mnasema
nyie ndio mnaojua kuimba mie
sijui “sinatatizo”… Mnasema nyie
ndio wenye sauti nzuri yangu
mbaya “Sina tatizo”… sasa
mbona tena bado mnanifatilia na
kutokujua kwangu… Nafkiri ni
vyema mkaanza kutumia ujuzi
wenu kukuza sanaa ya nchi yetu
na kuleta heshima na maendeleo
nchini, kuliko kupika majungu…..
Watu wanataka kazi! “

No comments:

Post a Comment