Monday, February 17, 2014

LULU AKUMBAKA MAPENZI YA KANUMBA VALENTINE‘S DAY

KAWAKATI kesi yake juu ya kifo cha aliyekuwa
nyota wa filamu Bongo, Steven Kanumba
ikianza kurindima leo katika Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam , mwigizaji Elizabeth
Michael ‘ Lulu ’ ametoa la moyoni
akikumbuka mapenzi ya jamaa huyo
aliyetangulia mbele za haki .
Elizabeth Michael ‘ Lulu’ .
Lulu alifunguka hayo mwishoni mwa wiki
iliyopita , Siku ya Wapendanao ( Valentine ’ s
Day ) iliyosherehekewa duniani kote Ijumaa
iliyopita .
Marehemu Steven Kanumba.
“ Kuna mtu natamani kumtakia Happy
Valentine ’ s Day kwa kuwa nakumbuka
mapenzi yake kwangu lakini kwa bahati
mbaya siwezi kwa sababu hayupo na
haiwezekani tena , ” alisema Lulu .
Hata hivyo, alipobanwa amtaje , staa huyo
ambaye ni sura ya mauzo ya filamu za
Kibongo alikiri kuwa ni Kanumba aliyefariki
dunia Aprili 7, 2012 , siku ambayo kamwe
hawezi kuisahau maishani mwake .

No comments:

Post a Comment