STAA wa sinema za Kibongo , amejikuta
katika wakati mgumu baada ya kufundishwa
mila za kimasai na kusema ameelewa, muda
mchache baadaye akachemka .
Tukio hilo lililogeuka kituko, lilitokea hivi
karibuni ambapo Chuchu akiwa na wasa
kilichopo mkoani Arusha kwenda kurekodi
sinema lakini alivutiwa na mavazi ya kimasai
ndipo alipoomba kujifunza mila za kabila hilo.
Akizungumza paparazi wetu, Chuchu alisema
alipewa mtoto mdogo amfundishe namna ya
kuvaa mavazi hayo ya Kimasai, akadai
ameweza lakini alipopewa mara ya pili avae
mwenyewe , alichemka .
“Daah! Niliabika maana mbaya zaidi
nilielekezwa na binti mdogo nikamwambia
tayari nimeweza lakini nilipokwenda kuvaa ,
nikavaa ndivyo sivyo, acha nichekwe , ”
alisema Chuchu .
watoto wa Kimasai .
Hata hivyo , baada ya kukosea huko, Chuchu
alisema alijifunza upya na kuhakikisha kuwa
ameweza hivyo kufuta aibu ya awali huku
akiwasisitiza wasanii wenzake kujifunza mila
tofautitofauti.
“Kujivunza mila tofauti ni jambo zuri katika
maisha yetu hususan sisi wasanii , tunatakiwa
kujua milia na tamaduni za kabila mbalimbali
ili kuyawakilisha katika sinema zetu, ” alisema
Chuchu.
No comments:
Post a Comment