Wednesday, February 19, 2014

BABY MADAHA ATANGAZA KUACHA MUZIKI,FILAMU

IKIWA imepita miezi kadhaa tangu anaswe
katika mtego wa kujiuza na makachero wa
OFM ya Global Publishers, staa wa Bongo,
Baby Madaha ametangaza kuachana na
sanaa ya muziki na filamu kwa maelezo
kuwa amechoshwa na maisha ya presha .
Baby Madaha.
Akistorisha na paparazi wetu juzikati jijini
Dar es Salaam , Madaha alisema ishu ile
imemsababishia matatizo makubwa ya
kifamilia na hata kibiashara, hivyo kujutia
mchezo mzima ulivyokuwa .
Alisema filamu anayoisambaza kwa sasa na
kibao chake cha mwisho kukitoa cha Mr. Dj
ndizo zitakazofunga pazia la mambo ya
sanaa kwa upande wake .
“ Nimeamua kuachana na sanaa kabisa ,
siwezi kuishi maisha ya presha yasiyo na
uhuru. Nitarudi kwenye fani yangu
niliyosomea (hakutaka kutaja) , maana naishi
maisha ambayo hayana amani kabisa , ”
alisema.
Hivi karibuni Madaha aliingia kwenye kumi
na nane za Oparesheni Fichua Maovu ‘ OFM ’
ya Global Publishers ambapo alipatana bei
ya kutoa uroda kwa ‘ mfanyabiasha’ wa
madini kutoka jijini Mwanza
aliyejitambulisha kwa jina la Mike – kumbe
ulikuwa mtego .

No comments:

Post a Comment