Sunday, January 19, 2014

Wastara Sajuki na Diana Kimaro ndani ya filamu moja

Msanii wakike wenye heshima kubwa bongo Wastara Sajuki ameingia ‘location‘leo kucheza filamu kama mama yake Diana kimaro

Wastara amesema filamu hiyo ameshirikishwa na kwamba jina lake ni supraizi mashabiki watarijua siku za mbele

“Hii filamu mimi nimeshirikishwa sio yangu na humu nimecheza kama mama yake Diana Kimaro na leo ndio tumeanza kushuti jina litatangazwa badae“

staa huyo ambae anagombewa kama dhahabu na waigizaji wenzie amesha cheza filamu mbili kutoka kwenye kampuni yake tangu marehemu mume wake afariki(Sajuki)ambazo ni Shaymaa inayofanya vizuri sokoni na “Last decision“ inayotarajia kutoka hivi karibuni na kushiriki nyingi zikiwemo Njia Panda,Mama Kijacho,Dokta Max na uaminifu dhaifu

No comments:

Post a Comment