Sunday, January 19, 2014

Kamata kamata ya Machangudoa yamkumba ‘bonge‘ambae ni mke wa mtu akiwa gesti

Kamatakamata na fumuafumua ya magenge ya biashara haramu ya ngono mjini Morogoro imemkumba bonge la jimama ambalo lilinaswa gesti likisubiri mteja.

Tukio hilo lilijiri hivi karibuni ambapo vijana wetu  walipata mwaliko maalum kutoka jeshi la polisi Moro kwa ajili ya kufichua biashara hiyo haramu ambapo mwanamke huyo alinaswa kauchapa usingizi chumbani huku kitandani kukiwa na kondomu kibao.

Ndani ya gesti maarufu ya Itigi iliyopo maeneo ya Msamvu, inayotumiwa zaidi na madereva wa malori ya masafa marefu ndipo alipobambwa bonge ambaye katika utetezi wake alidai kuwa ni mke wa mtu.

Hata hivyo, pamoja na utetezi wake, bonge aliunganishwa na wenzake walionaswa kisha akapewa henyahenya na polisi kabla ya kutupwa nyuma ya nondo za mahabusu kusubiri sheria kuchukua mkondo wake.

GP

No comments:

Post a Comment