Friday, January 10, 2014

Sandra na rushwa ya ngono

STAA wa filamu Bongo, Salma Salmini ‘Sandra’ amesema kuwa tangu ajiunge Bongo Movie hakuna manufaa aliyoyapata kwa kuwa chama hicho kinaendekeza ubaguzi kwa kuthamini rushwa ya ngono.

Akipiga stori na paparazi wetu alisema, kikubwa kinachoikwamisha tasnia hiyo ambayo kwa sasa inaongozwa na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ni watu kusaidiana wenyewe kwa wenyewe kwa kuwa labda wanatoka kimapenzi au kutegemea kupewa rushwa ya ngono ili impe shavu mtu.

“Namsihi sana huyu kiongozi wetu wa sasa awe makini na hili suala, yeye pamoja na utawala wake wote wapinge haya mambo na tushikamane ile kuleta maendeleo, maana kila siku wanaopewa madili ya maana ni walewale lakini wengine tunaheshimika kwa majina tu huku dhiki zikitutawala,” alisema Sandra.

GP

No comments:

Post a Comment