Monday, January 13, 2014

Monalisa:hofu ya juju

STAA wa filamu Bongo, Yvone Cherry ‘Monalisa’ amesema anaogopa kuweka wazi mambo yake kwa kuhofia kupigwa juju hivyo anaishi kwa siri.

Akipiga stori na paparazi wetu, Monalisa alisema amejifunza maisha ya usiri na ndiyo maana huwa haaniki hata tarehe, mwezi au mwaka wa kuzaliwa kwani watu wabaya hutumia nafasi hiyo kukuangamiza.

“Asikudanganye mtu ukishaanika tu hivyo vitu mtu akajua na majina yako yote kuna nini tena hapo zaidi ya kukufanyia ndumba uharibikiwe anavyojisikia yeye, huwa inaniwia vigumu sana kuweka hadharani vitu vyangu,” alisema Monalisa.

No comments:

Post a Comment