Thursday, December 12, 2013

Familia ya mzee Small ya kanusha taarifa za uongo zinazodai amefariki dunia

Ni mastaa zaidi ya 10 wa Tanzania ambao wamezushiwa kifo ndani ya mwaka 2013 na stori zote zikawa za uongo baadae, miongoni mwao ni Mwasiti na Mr Blue.

December 10 2013 kuanzia saa nne usiku taarifa zilezile za kuzushiwa kifo zimemuangukia mwigizaji mzee Small ambae ni kweli kwa kipindi kirefu amekua akiugua.

Hii  ni  kauli  ya  msanii  huyo  baada  ya  kutembelewa  na Millard Ayo  nyumbani  kwake.

1. Bado yuko hai ila ana maumivu ya bega na mkono kutokana na mshtuko alioupata toka May 2012.
 
2. Anasema ‘mlitaka kwenda kuchukua jeneza kutokana na taarifa za kifo cha uongo lakini sasa msichukue, hiyo pesa ya sanda hiyo mchukue mkanunulie watoto chakula wale’
 
3. Usingizi wao usiku wa kuamkia December 11 2013 ulikua wa tabu sana, wamepigiwa simu zaidi ya 10 za watu mbalimbali hata usiku wa manane wakitaka kujua ukweli wa taarifa za kifo.
 
4. Familia ya Mzee Small inakiri hii ni mara ya pili kwa mwigizaji huyu kuzushiwa kifo ila ya mara hii ndio imekua kubwa kuliko.
 
5. Mzee Small anasema ‘misaada ya Watanzania kwa njia mbili kaka, kwanza dua zao ndio maana sikufa… mimi sijafa bwana, mimi mzima kabisa, nawashukuru Watanzania

No comments:

Post a Comment