Friday, July 11, 2014

ROSE NDAUKA AMKIMBIA MUMEWE, KISA MFUNGO


Staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka hivi karibuni aliamua kumkimbia mumewe Malick Bandawe, kisa mfungo wa Ramadhani ambapo sasa anaishi Kigogo na mama yake mzazi.


 Rose alisema amelazimika kwenda nyumbani kwao ili kumpisha mumewe atimize nguzo hiyo ya Uislam bila kipingamizi kutokana na kutokufunga ndoa.
 “Mimi sifungi hivyo nimeona pia ni jambo la busara kumpa nafasi mwenzangu kwa ajili ya kufanya ibada hiyo, mwezi ukiisha nitarudi na maisha yetu yataendelea kama kawaida,” alisema Rose ambaye awali alikuwa akiishi na mumewe huyo Tandale jijini Dar.

No comments:

Post a Comment