Friday, July 11, 2014

SANDRA AKUMBUSHIA MATESO YA KAOLE

MUUZA sura wa sinema za Kibongo, Salma Salmini ‘Sandra’ ametoa dukuduku lake baada ya kuelezea mateso aliyopata kipindi alipokuwa anaanza kujihusisha na masuala ya sanaa katika Kundi la Kaole.



Sandra amesema kuwa, mateso anayoyazungumzia ni yale ya kunyanyaswa na wasanii wenzake huku wakimfanyia vitimbi vya kila aina ili asifikie malengo yake lakini anamshukuru Mungu aliweza kuhimili.
“Kila nikikumbuka roho inaniuma maana kuna watu walikuwa na chuki na mimi za waziwazi, walitamani wanitoe roho. Kusema kweli niliteseka mno mpaka kupata nafasi ya kuanza kuonekana kwenye runinga na kufikia hapa nilipo,” alisema Sandra.

No comments:

Post a Comment