MUIGIZAJI Bora wa Kike 2014 kupitia Tuzo za Zanzibar
Film Festival (Ziff), Esha Buheti ameapa kuwa iwapo atakuja kujichora
tatuu au kufanya mapenzi ya jinsia moja, Mungu aingamize familia yake na
kizazi chake chote.
Esha alitoa kiapo hicho juzikati alipokuwa akijibu swali aliloulizwa na
paparazi wetu kuhusiana na tuhuma za kudaiwa kujihusisha na mapenzi ya
jinsia moja zilizotua kwenye dawati la Risasi Jumamosi.
“Mimi ni
mtoto wa Kiislamu na nina maadili yote ya dini, siwezi kujihusisha na
mapenzi ya kinyume cha maumbile, mapenzi ya jinsia moja,” alisema.
No comments:
Post a Comment