Mtangazaji wa Kipindi cha The One Show, Jokate Mwegelo ‘Jojo’ amefunguka
kuwa hahusiki na kuvunjika kwa ndoa ya Khadija Shaibu ‘Dida’ kwani ni
mshikaji wake na wanaheshimiana.
Akijibu tuhuma kuwa, yeye anahusika na kuparaganyika kwa ndoa hiyo
kufuatia ‘ku-fall in love’ kwa mume wa Dida, Edzen Jumanne ambaye ni
mtangazaji mwenzake, Jokate alisema:
“Yaani watu wanapenda kuungaunga maneno kweli, jamani mimi siwezi hata
siku moja kuwa na Edzen, ni mfanyakazi mwenzangu halafu Dida ni mshikaji
wangu siwezi kabisa, tena wasitake kunitibulia.”
chanzo Global
No comments:
Post a Comment