MSANII maarufu katika tasnia ya filamu Bongo, Sabrina
Rupia ’Cathy’ amewataka wasanii wenzake kutofanya ustaa kwenye ndoa zao
kwani ndiyo chanzo cha kuvunjika kwa ndoa nyingi.
Akipiga stori na paparazi wetu, Cathy alisema kabla ya kuolewa lazima
uwe na utayari wa kuolewa na kujuana kwa undani zaidi na mwenzio kabla
ya kufanya uamuzi pia usiweke neno kuachika katika ndoa kwa sababu tu
unaweza kupata mwingine.
“Uvumilivu ndiyo nguzo muhimu katika ndoa, unapojifanya staa na
kuishi maisha ya kistaa katika ndoa, mambo yanaharibika kabisa,” alisema
Cathy huku akikataa kutoa mifano ya walioachika kwa kuendekeza ustaa
katika ndoa akidai wanajijua.
No comments:
Post a Comment