Sunday, February 02, 2014

Jokate amfanyia “suprise“ wema

Jokate na Wema historia yao ilianzia kwenye
shindano la kumtafuta Miss Tanzania 2006
ambapo Mshindi alikua ni Wema Sepetu
akifatiwa na Jokate kisha mshindi wa tatu akiwa
Lissa Jensen.
Vichwa vya habari vilikuja kutengenezwa tena
vikiwahusisha warembo hawa kuonekana wako
na mtu mmoja ambapo magazeti na mitandao
mingi iliandika mahusiano haya yaliyokua
yakimhusu Diamond Platnumz kutoka na
warembo hawa.
Kimepita kimya kirefu sana juu ya hawa watu
wawili hadi usiku wa February 01 huko Arusha
kwenye Tamasha la Divaz Night Endless Fame
ambalo ndani yake kulikua na mastar kadhaa
akiwemo Wema Sepetu,Aunt Ezekiel,Martin
Kadinda,Kajala,Zamaradi Mketema,Chid
Benzi,Mirror,Jordan na wengine kibao.
Wakati Madam Wema Sepetu akimwaga mauno
kwenye jukwaa bila kutegemewa na mtu yoyote
Jokate alipanda Jukwaani na kuanza kumtunza
Wema pesa na wakati huo Wema alikua akicheza
Wimbo wa Diamond My Number One ‘Ngololo’
ambapo Jokate aliungana na Wema kuucheza
Wimbo huo.

No comments:

Post a Comment