Thursday, January 30, 2014

SHILOLE ANASA KWA MZUNGU

KWA mara ya kwanza msanii wa filamu na
muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole ’
amenaswa akiwa na mwanaume wa Kizungu
anayedaiwa kuwa ndiye mchumba wake .
Zuwena Mohamed ‘ Shilole’ akiwa na
mchumba wake .
Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa,
safari za mara kwa mara za Shilole nchini
Uingereza zimekuwa zikisababishwa na
mchumba huyo wa Kizungu ambaye huwa
anamuita kufurahia penzi lao pamoja na
kumtafutia shoo mbalimbali .
“ Ukweli ni kwamba Shilole ana mchumba
wa Kizungu na walikutana kwenye shoo ya
mara ya kwanza aliyoenda kufanya nchini
Uingereza na hivi karibuni ataenda tena na
amealikwa na huyo mchumba wake , ”
kilisema chanzo hicho.
Gazeti hili limekuwa la kwanza kunasa picha
kadhaa za Shilole akiwa katika mapozi
tofauti ya kimahaba na Mzungu huyo .
Baada ya chanzo hicho kumwaga ‘ upupu ’
huo, mapaparazi wetu walimtafuta Shilole ili
aweze kufunguka ambapo bila kuumauma
maneno, alikiri kuwa amepata mchumba
huyo aliyemtambulisha kwa jina la Ankar .
Akizidi kumwaga data za boifrendi wake
huyo , Shilole alisema awali walikutana
kwenye moja ya shoo zake nchini humo
ndipo urafiki ulipoota mizizi na kufikia hatua
ya kuwa wapenzi.
“ Kweli nina mchumba Mzungu ambaye ni
raia wa Uingereza, nilipokuwa napataka
nimefika , sipindui tena. Unajua muziki
wangu na mauno yangu yanawavutia sana
watu , siku ya kwanza aliniona kwenye shoo
akanipenda ndipo tukaanzisha urafiki .
“ Hivi karibuni nina safari ya kwenda nchini
humo kwa mwaliko maalum alionipa,
nitaenda peke yangu kwani safari nyingine
zote zilizopita nilikuwa naenda na watu , ”
alisema Shilole

GP

No comments:

Post a Comment