STAA wa Bongo Movie, Halima Yahaya
‘Davina ’ amefunguka kuwa mwaka 2013
aliutumia zaidi kwa kulea mimba hadi
kujifungua hivyo kukosa madili ya kazi za
uigizaji.
Akizungumza na paparazi wetu , Davina
alisema mwaka huu amejipanga kurejea
upya katika sanaa kwani amegundua kuwa
mashabiki wake walikuwa wamemmisi hivyo
lazima apambane kutetea taito yake katika
sanaa.
“ Nimejipanga zaidi mwaka huu ,
nimedhamiria kufanya mapinduzi makubwa
katika sanaa tofauti na kipindi cha nyuma ,
kulea siyo mchezo ilibidi sanaa ikae
pembeni kidogo, ” alisema Davina ambaye
sasa ni mama wa mtoto mmoja , Fazal.
GP
No comments:
Post a Comment