Mcheza filamu za kibongo mwenye sifa ya kuitendea haki “scene“ya kulia Riyama Ally amesema aliamua kuingia kwenye sanaa ili kupoteza mawazo ya kufiwa na mtoto wake wa kwanza.
Akiongea na blog hii Riyama amesema sanaa aliipenda sana tangu zamani ila hakuwa tayari kuifanya kutokana na majukumu mengine ikiwemo kulea mtoto lakini mtoto wake alipofariki akaingia kwenye sanaa ili kuondoa mawazo na upweke.
“Niliingia kwenye kupoteza mawazo badala ya kufiwa na mtoto wangu wakwanza upweke ulinifanya nikajumuike na wenzangu mungu akabariki leo imekua kazi yangu asante mungu na mashabiki kunipokea“
Riyama sasa amebahatika kupata mtoto mmoja wa kike anaitwa Fatma picha chini ni Riyama akiwa na mtoto wake Fatma
No comments:
Post a Comment