NYOTA
wa filamu na mshindi wa zamani wa Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike
nchini, Riyama Ally a.k.a Riyama amewataka wasanii wenzake kuacha tabia
alizoziita za kijinga kwa kuiga maisha na uigizaji wa wasanii wa
ng’ambo.
Riyama ambaye sifa yake kubwa kwenye ‘game’ ni kuvaa
uhusika, hasa wa kumwaga machozi, alisema hayo hivi karibuni katika
mahojiano maalum na gazeti hili jijini Dar es Salaam.
“Usanii
si kukaa uchi, unajua baadhi ya wasanii wenzetu wanashindwa kufahamu
hilo. Kukaa uchi hakumaanishi ndiyo utaonekana mzuri zaidi,” alisema kwa masikitiko Riyama.
Akizidi
kushusha ‘maskadi’ Riyama alisema, tatizo kubwa walilonalo wasanii wa
Kibongo ni kuiga, mwenyewe anafafanua: “Haijakatazwa kuiga, lakini
unatakiwa kujua unaiga nini. Hatuwezi kuchukua tamaduni za watu na
kuleta kwetu. Wao wana miiko yao, nasi pia. Kwanini tuige ujinga?”
Alisema,
wasanii kuvaa nguo fupi zisizo na heshima, huua soko la filamu bila la
wasanii wenyewe kujua kwani watu wenye heshima zao hawawezi kununua na
kwenda nazo majumbani mwao
No comments:
Post a Comment