"Maneno ya watu ndo yaliyonifanya nikubali kulala na bosi wangu....Walinisema sana, nikaamua kufanya kweli"....Baby Madaha
Hivi sasa sio siri tena wala Baby Madaha hataki tena kupindisha pindisha maneno kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na meneja wake wa Kenya CEO wa Candy n Candy Joe Kariuki.
Msanii huyo filamu na muziki kutoka Tanzania Baby Joseph Madaha, ameiambia Global kuwa mwanzoni yeye na Kariuki hawakuwa na uhusiano wa kimapenzi zaidi ya kazi, ila kutokana na watu kuanza kuongea kitu ambacho hakipo ndio kilichopelekea kuamua kufanya kweli..
“Kusema kweli huyu kaka kanikoleza jamani japo watu watachonga mengi lakini abadani sitosikiliza maneno yao, kwa kuwa awali sikuwa na uhusiano naye ila porojo za watu zilipelekea kuchukua maamuzi hayo, natamani nihamie Kenya ili tuwe karibu wakati wote,”alisema Baby Madaha.
Novemba 5 mwaka huu Baby Madaha alizikana tetesi zilizokuwepo wakati huo za uhusiano kati yake na Kariuki.
“Joe amesikia na hajapenda hili swala kwasababu sisi tupo kikazi zaidi na siyo mambo mengine kama wasemavyo wao”, alisema Madaha katika mahojiano hayo.
Madaha pia ameongeza kuwa ameamua kuwa na Kariuki kutokana na upendo anaomuonesha na si uwezo wa kipesa kama wengi wanavyodhani.
No comments:
Post a Comment