Sunday, December 01, 2013

Nisha:Shaymaa ni movie ambayo nimeonesha kipaji changu chote na cha ziada

Mrembo anaekuja juu kwa kasi kwenye filamu za kibongo Salma Jabu Nisha amewataka wapenzi wa filamu kuinunua filamu mpya ya Wastara Sajuki inayoitwa Shaymaa ili waone alichokifanya

Nisha amesema kwenye filamu hiyo inayotoka mwanzoni mwa mwezi huu amecheza kama Shaymaa na ameonesha kipaji chake chote na cha ziada

“kama kawaida sijawaangusha.. ni movie ambayo nimeonesha kipaji changu chote na cha ziada.. huchoki kuitazama.. rika zote.. tumezingatia sana maadili kikubwa mkiiona ndio mtathibitisha.. maneno hayatoshi.. ila vitendo vinaongea kwa sauti“

Amesema watanzania wasapoti kwa kununua nakala halisi na kuacha uchakachuaji kwani unawarudisha nyuma kwenye kazi zao

No comments:

Post a Comment