Friday, August 22, 2014

HAKUNA KAMA WASTARA BONGO MOVIE,ALICHOKIFANYA NI ZAIDI YA HISTORIA

Mcheza filamu mwenye sifa ya kuzitendea haki filamu za huzuni Wastara Juma  ameandika historia nyingine kwenye maisha yake ya sanaa baada ya kufanya uzinduzi wa filamu yake mpya ya Last Decision mtaa kwa mtaa tofauti na wasanii wenzake amabo wanaziundua kwenye kumbi za starehe
Akiongea kiafrika bila hofu yoyote kwa kua Tanzania ni inchi huru Wastara amesema anatambua thamani ya mashabiki wake na kua wengi wao ni wa hali ya chini kifedha hivyo ameomua kufanya mtaani ili wauone tofauti na kwenye kumbi wangeudhulia wachacwenye nazo
'nimeamua kufanya hivi ili kuwafikia mashabiki wangu wote na kuwauzia cd kwa mkono wangu nikiwa sambamba na team yangu team wastara"

Nae meneja wa Wastara Bond Bin Sinnan amesema anafuia sana kufanya kazi na mrembo huyo kwani anashaurika na anatambua anachokifanya kwenye tasnia ya filamu,vilevile amewapongeza team wastara kwa moyo wao wakujitolea kusapoti Wastara

filamu ya Last DEcision imezinduliwa 14.08 mwaka huu na kusambaa nchi nzima kupitia kampuni ya steps

No comments:

Post a Comment