Saturday, August 23, 2014

NORA AWABOMOA BONGO MOVIE

MKONGWE kwenye kilinge cha filamu Bongo, Nora amewachana viongozi wa Bongo Movie kwa kuwasahau wakongwe kwenye gemu.

Nora ambaye ni zao la kundi la maigizo la Kaole, alisema wasanii wa klabu hiyo ambayo wameibuka miaka ya hivi karibuni, wamekuwa wakijitokeza katika kila idara inayohitaji wasanii pasipo kuwashirikisha wakongwe waliotokea kwenye makundi.
Alisema wasanii hao hawana baraka za wasanii wakongwe lakini wamekuwa mstari wa mbele kupata ‘mashavu’ makubwamakubwa.
“Wanapotosha sanaa ya kweli, tasnia inaonekana ya wahuni kitu ambacho kinatushusha kwa hao watu ambao tunawaomba watusaidie,” alisema Nora.

No comments:

Post a Comment