Friday, August 22, 2014

TUACHE KUCHOCHEA BIFU KILA KUKICHA INABOA

Tanzania imejaliwa kuwa na wanamuziki wengi wazuri na wenye vipaji vya hali ya juu kwenye utunzi na kuimba,lakini siku za hivi karibuni kumekua na ushindani wa mashabiki wakichochea bifu kati ya Diamond na Alikiba jambo ambalo wenyewe wanakana kuwa na bifu na kati yao

Ni ukweli usiofichika Diamond ndio msanii pekee kwa sasa anaeonekana anafanya vizuri kimataifa na kuitangaza nchi yetu lakini ikumbukwe kuna wanamuziki wengi sana wanauwezo wa kuimba na wakafika mbali hivyo tuache uchochezi wa kutaka kuwa gombanisha wanamuziki wetu badala yake tusapoti kazi zao

Alikiba anafanya vizuri kwa nafasi yake na Diamond anafanya vizurui kwa wakati wake vile vile kuna wanamuziki kama Linex,Rich Mavoko,Barnaba,Ben Paul,Amin nao wanafanya mziki huu ila inashangaza sana kuwa na ushabiki wa watu wawili tu je ni kweli wenyewe ndio wanafanya vizuri kwa sasa?

tusapoti mziki wetu ufike mbali

No comments:

Post a Comment