MUIGIZAJI aliyelamba tuzo ya Muigizaji Bora wa Kike
katika Tamasha la Zanzibar Festival Film ‘ZIFF’ mwaka huu, Esha Salim
Buheti hali yake siyo nzuri na anahitaji maombi ili apone kutokana na
kusumbuliwa na tatizo la uvimbe kwenye kizazi.
katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni jijini Dar, Esha alisema,
alifikishwa hospitalini hapo juzi Jumatano akiwa na hali mbaya kufuatia
‘kuendesha’ ile mbaya.
“Nilifikishwa hapa nikiwa na hali mbaya, nilikuwa ‘naendesha’ sana
hadi kufikia hatua ya kuishiwa nguvu, ilibidi wanichukue vipimo ili
kujua tatizo
“Baadaye wakaniambia nina uvimbe kwenye kizazi na UTI, yaani dah! Naomba
Mungu anisaidie na naomba mashabiki wangu pia waniombee nipone,”
alisema Esha.
No comments:
Post a Comment