Mwanamuziki
maarufu wa nchini Uganda, Juliana Kanyomozi, leo asubuhi amempoteza
mtoto wake mdogo wa kiume Keron baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa Pumu.
Kwa mujibu wa gazeti na New Vision Keron amefariki katika hospitali ya
Aghakhan.
Ni wakati mgumu kwa mwanamuziki huyo mrembo kwakuwa amekuwa akimpenda sana mtoto wake wakati akithibitisha taarifa hizo.
New
Vision imemnukuu Juliana akisema kuwa” Malaika wangu ametangulia kwa
Mungu, kilichosambazwa awali ni uzushi. Amefariki leo saa 10:25 asubuhi
hii, amekuwa mpambanaji mkubwa wa afya yake nawashukuru wote kwa maombi
yenu nitajitahidi kujikaza, Mungu amlaze mahali pema Keron lala salama
mwanangu hadi tutakapokutana tena.”
Juliana amewaomba mashabiki wake kumuombea mtoto wake huyo haswa katika kipindi hiki kigumu kwake.
Juliana amesema mtoto wake hakuwa katika hali nzuri baada ya kushambuliwa na ugonjwa wa Pumu uliomsababishia kupoteza maisha.
No comments:
Post a Comment