Marehemu
Geogre Tyson pichani hapa alikuwa yupo kijiji cha Chilonwa Chamwino
kwenye utoaji wa madawati katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma.
Baada ya kumaliza shughuli hii huku akiwa kama producer wa The Mboni
Show mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni masaa 4 tu toka Kuanza
safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia
GAIRO mjini.
Katika gari
hilo walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza mauti na wengine
kupata majiraha mwilini pamoja na dereva wa gari hilo. Kwa sasa mwili wa
marehemu umehifadhiwa mjini Morogoro katika hospital ya mkoa Morogoro,
asubuhi hii mwili unategemewa kusafirishwa kurudi Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment