MAMA mzazi wa marehemu Hussein Mkiet‘Sharo Millionea ’ , Bi. Zuwena Mkieti
amewataka waandaaji wa filamu za
Kitanzania kusitisha mara moja matumizi ya
sinema za mwanaye huku akishusha
lawama nzito .
Akizungumza kwa njia ya simu na ‘kiranja ’
wetu mwanzoni mwa wiki hii, mama huyo
alidai kujisikia uchungu kuona kazi za
mwanaye zinazidi kuingia sokoni huku
familia yake ikiambulia patupu .
“ Ninasikitika sana kuona kuna muvi ambazo
zinatoka ndani yake amecheza Sharo , sina
taarifa yoyote hivyo naomba wasitishe mara
moja au vinginevyo waje kwangu
tuzungumze kabla ya kuingiza kazi za
mwanangu sokoni ili nami nipate angalau
chochote , ” alisema Mama Sharo .
GP
No comments:
Post a Comment