Penny ambaye ni mpenzi wa zamani wa Naseeb Abdul "Diamond" haonekani kujutia kitendo cha kumwagana na msanii huyo na badala yake sasa ameanza kuzipa uzito hoja za kumpiga chini Diamond ambaye walidumu naye kimapenzi kwa takribani mwaka mmoja....
Kwa mujibu wa watu wa karibu na Penny, kitendo cha Diamond kumpandisha jukwaani Wema Sepetu pale Leaders Club kilipata kila aina ya laana toka kwa mama mzazi wa Diamond kwani hakuridhia jambo hilo.....
"Mama alilalamika sana kuhusu Diamond kumpandisha Wema pale leaders Club, kimsingi ni kwamba hataki kabisa uhusiano kati ya Diamond na Wema Sepetu"...Kilisema chanzo kimoja ambacho ni rafiki damu na familia hiyo.
Wakati hayo yakijitokeza ndani ya familia ya Diamond, kwa upande wa Wema, mama yake pia anadaiwa kulalamikia kitendo cha mwanaye kutumika kila mara kumbusti Diamond pale umaarufu wake unaposhuka...!
"Mama Wema naye analalamika mwanaye kutumika kama daraja la kuwavusha watu kwenye umaarufu halafu wakishafanikiwa wanamgeuka na kumdhalilisha, kifupi ni kwamba hataki kabisa kusikia mahusiano ya Wema na Diamond" Kilifunguka chanzo hicho.
Aidha imeelezwa kuwa Diamond amekuwa akimpgia simu Penny mara kwa mara kumuomba wayamalize lakini Penny amekuwa akimjibu kwa kifupi kuwa "Nimekuachia Wema Wako"
Taarifa nyingine toka vyanzo vya kuaminika zinaeleza kuwa Penny amekuwa akijisifu kuachana na Diamond kwa hoja kuu tatu:
Moja: Kuondokana na skendo zisizo na faida kwake.
Pili: Kupunguza malalamiko toka kwa familia yake.
Tatu: Penny aliingia katika mahusiano na Diamond si kwa ajili ya mapenzi, bali kulipa kisasi kwa Wema ambaye aliwahi kumchukulia mpenzi wake.
"Hata kutoa mimba ya Diamond amekuwa akisema kwamba kama angezaa naye watoto wake wangekuwa na sura mbaya na midomo ya ajabu".Kilimalizia
No comments:
Post a Comment