Wednesday, January 15, 2014

Mama Kanumba:Lulu ni mkwe sahihi kwangu

MAMA wa marehemu Steven Kanumba, Frola Mtegoa ameibuka na kueleza kuwa, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ni mkwe sahihi kwake kwa namna alivyo na heshima na anavyomjali kama mama yake.

Mama mzazi wa marehemu, Steven Kanumba, Flora Mtegoa akipozi na Lulu.

Akizungumza wikiendi iliyopita nyumbani kwake, Kimara - Temboni, Dar, mama huyo alisema, kama mwanaye angekuwa hai angekuwa amepata mke bora wa maisha yake, naye pia alikuwa na mkwe sahihi.
“Najua mtoto wangu ametangulia mbele za haki lakini faraja anayonipa Lulu ni kubwa mno na  najisikia furaha. Kama Mungu angemwacha Kanumba hai mpaka leo kwa kweli Lulu angekuwa mkwe bora sana kwangu.

“Sina jinsi, ndiyo imeshatokea lakini mimi kama mzazi bado nitaendelea kumpenda na kuwa bega kwa bega na Lulu hata akipata mchumba mwema wa kumuoa, sina tatizo na hilo... namwombea sana kwa Mungu huyu binti,” alisema kwa hisia mama Kanumba.

GP

No comments:

Post a Comment