Saturday, December 21, 2013

Sasa hii ni rasmi Diamond vs Penny live chanzo chadaiwa kuwa ni Wema

SASA HII NI RASMI DIAMOND
Vs PENNY LIVE, CHANZO
CHADAIWA KUWA NI WEMA
NDIYO habari ya ‘mujini’ kwa sasa, kwamba staa
wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond
Platnumz’ na mwandani wake, mtangazaji wa
kituo cha runinga cha DTV, Penniel Mungilwa
‘Penny’ wamemwagana, Risasi Jumamosi
limemwagiwa upupu.
Penniel Mungilwa ‘Penny’
na Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’.
KAMA UTANI, WEMA ATAJWA
Kwa sharti la kutotajwa mahali popote, ‘mtonyaji’
wetu ambaye ni mtu wa karibu wa wawili hao
aliliambia gazeti hili kuwa chanzo cha Diamond
na Penny kuingia kwenye listi ya ‘zilipendwa’
kilianza kama utani.
Awali ilidaiwa kuwa kila mmoja amekuwa akijiona
mwenye thamani mbele ya mwenzake huku
Wema Sepetu naye akidaiwa kuwa chanzo.
Nasibu
Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ akiwa na
Wema Sepetu.
“Hakuna penzi tena kati yao, wameachana na
kila mmoja yuko kivyake.
“Walianza kama utani, unajua wale kila mmoja
anajiona yuko juu kuliko mwenzake, lakini
kitendo cha Diamond kuripotiwa kutoka na
wanawake tofauti mara kwa mara hasa Wema,
kimemchosha Penny ndiyo maana ameamua
kujiweka pembeni kuepuka msongamano.
“Kupangwa kama mafungu ya nyanya inahusu?”
alihoji ‘kikulacho’ huyo ambaye ni rafiki wa
Diamond.
RISASI MZIGONI
Baada ya kutojiridhisha moja kwa moja na taarifa
za awali kutoka kwa rafiki huyo, timu ya gazeti
hili kwa kuwatumia ‘wahangaikaji’ wake maalum,
iliingia mzigoni kupeleleza ukweli juu ya tetesi
hizo.
Watu kadhaa walio chini ya Wasafi Classic Baby
(WCB) ambayo rais wake ni Diamond walihojiwa
ambapo majibu yalikuwa yaleyale kwamba, kwa
sasa Diamond na Penny imebaki stori!
SHAKA ILIPOANZIA
Wakati timu yetu ikiendelea na uchunguzi wake
makini juu ya uvumi huo, hivi karibuni Diamond
alionekana ‘singo’ kwenye pati ya kusherehekea
siku ya kuzaliwa ya ‘dada wa mjini’, Halima
Haroun ‘ Halima Kimwana’ ambayo aliiandaa
Diamond.
Minong’ono ya kuhoji kutoonekana kwa Penny
ilisikika ndani ya Ukumbi wa Business Park,
Kijitonyama jijini Dar ilikofanyikia pati hiyo iliyojaa
vitendo vya ufuska.
“Haiwezekani leo rais (Diamond) akajiachia peke
yake bila Penny. Si kawaida ya Diamond.
“Kwa vyovyote watakuwa wameshamwagana
kwa sababu kwenye pati zote huwa wanakuwa
pamoja tangu walipoanza uhusiano wa
kimapenzi,” alisikika mmoja wa waalikwa katika
sherehe hiyo.
Katika tukio hilo, Penny alipigiwa simu na
paparazi wetu na kujibu kwa kifupi: “Naumwa.
Halafu si lazima nije kwani kila mtu ana ratiba
zake.”
Penniel Mungilwa ‘Penny’.
PENNY KIZIMBANI TENA
Baada ya kukamilisha udadisi huo kupitia kwa
watu wao wa karibu, gazeti hili lilianza na Penny
kwa kumuuliza undani juu ya habari hiyo lakini
alionekana kuwa ‘mzito’ kwa kutoingia ndani
kulizungumzia sakata hilo huku akiahidi
kulifungukia muda wowote kuanzia sasa.
“Kwa sasa sina cha kuzungumza juu ya hilo,
nitalizungumzia muda wowote tena si siku nyingi
zijazo, lakini si leo, tafadhali sana,” alijibu Penny
kwa kifupi na sauti ya chini iliyojaa uchovu.
Paparazi: “Hebu nisaidie, mko wote au hamko
wote?”
Penny: “Nimesema sitoweza kusema lolote kwa
leo, subirini.”
                         Nasibu Abdul Juma ‘Diamond
Platnumz’.
DIAMOND KIMYA
Alipotafutwa Diamond kwa njia ya simu yake ya
kiganjani, hakupokea licha ya kupigiwa mara
kadhaa kwa namba zake zote. Akatumiwa meseji
yenye maelezo yote, hakujibu.
MAMA DIAMOND
Ili kujiridhisha na madai hayo, waandishi wetu
walimtafuta mama mzazi wa Diamond, Sanura
Kassim ‘Sandra’ ambaye alisema hajui na hana
taarifa hizo.
NDUGU WA KARIBU SANA
Baada ya mama Diamond, paparazi wetu
alimpigia simu ndugu wa karibu sana na
Diamond, sikiliza:
Paparazi: “Kumbe Diamond na Penny
wamemwagana we huniambii. Sasa wifi yako
mpya ni nani?”
Ndugu: “Aka! Sikwambii. Kwanza mi nipo mbali,
sipo Dar.
WADAU WANAJUA
Haikuishia hapo, timu yetu ilizungumza na
wadau mbalimbali ambao walionesha kusikitika
huku baadhi yao wakisema walitabiri tangu awali.
“Duh! Penny ameachia ngazi mwenyewe. Sisi
tulijua hawawezi kufika mbali, maana penzi
lenyewe lilikuwa na mbwembwe nyingi,” alisema
mwanamke mmoja anayejua kila kitu.

Risasi

No comments:

Post a Comment