Msanii wa filamu Kajala Masanja atahukumiwa upya Novemba 25 mwaka huu baada ya mumewe kukata rufaa.
Kesi iliyokuwa ikiwakabili wanandoa hao ilihusiana na utakatishaji wa fedha haramu uliofanywa na mume wa Kajala wakati akifanya kazi kwenye Benki ya NBC, Dar.
Habari za ndani zinaarifu kuwa, Kajala alisharidhika na hukumu iliyotolewa Machi 25, mwaka huu ambapo yeye alitakiwa kufungwa mitatu au kulipa faini ya shilingi milioni 13.
Katika hukumu hiyo, mume wa Kajala alifungwa miaka saba na ndipo alipoamua kukata rufaa na akamuingiza Kajala kwa maelezo kuwa wote hawakuridhishwa na hukumu iliyotolewa mwanzoni.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Kajala, staa huyo amekuwa katika wakati mgumu na mara nyingine na kujikuta akiangua kilio hasa anapokumbuka maisha ya gerezani.
Aidha, hukumu ya rufaa hiyo ilibidi isomwe juzi katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam lakini iliahirishwa baada ya Jaji aliyetakiwa kusoma hukumu hiyo kupata hudhuru
No comments:
Post a Comment