Muigizaji wa filamu za kibongo Happy Nyatawe amesema anatamani siku moja awe kama Wastara Sajuki na Salma Jabu kwa kufanya kazi zake mwenyewe akiwa na kampuni yake
Nyatawe amesema hayo wakati akiongea na blog hii na kuongeza kua atajitaidi kufanya filamu zake kama wanavyo fanya mastaa hao hivyo wapenzi wake wasubiri kuona kazi zake
Akiongelea wasanii anaowapenda kazi zao amesema msanii wa kiume alikua marehemu Juma Kilowoko (Sajuki)na wa kike ni Monalisa
Mbali na hayo nyatawe anafanya biashara ya kuuza nguo na viatu anatoa Afrika kusini na kuleta hapa nchini
Amesema hawezi kutegemea sanaa peke yake ni lazima awe mjasiliamali
No comments:
Post a Comment