Wednesday, December 31, 2014

MIAKA 2 YA KIFO CHA SAJUKI WASTARA AMEFUNGUKA MAZITO MTANDAONI

Kupitia ukurasa wake wa facebook na Instagran mcheza filamu za kitanzania Wastara Juma amefunguka haya hapa,hii ni ikiwa zimebaki siku chache asome kisoma cha marehemu mume wake Sajuki

 "mbali nami mpenzi umekwenda moyo wangu jeraha umeweka,sura yako aijanitoka nikifikilia machozi yanitoka,baby wangu rudi,

Ijumaa ya 02.01.2015 kutakuwa na kudhuru kaburi la marehemu mume wangu Juma Kilowoko (sajuki) kwenye makaburi ya kisutu muda ni saa 4 asubuhi,pia baada ya hapo kutakuwa na kisomo na chakula cha mchana nyumbani tabata,naomba tuungane pamoja kumuombea kipenzi changu,kipenzi chenu,kipenzi cha watanzania wapenda filamu,asanteni
02.01.2015 Marehemu mume wangu kipenzi Juma Kilowoko (sajuki)anatimiza miaka 2 tangu atuache tukiwa na majozi tele moyoni mwetu,

ni ukweli usipoingika ameondoka na nusu ya akili yangu maana sifanyi chochote bila kumfikilia yeye kwa jinsi alivyokua na mawazo mazuri ya kujenga namkumbuka na nitamkumbuka siku zote za maisha yangu,nampenda na nitampenda siku zote,

Hivyo 02.01.2015 kutakuwa na dua itakayosomwa kwenye kaburi lake kisutu Dar es salaam kuanzia saa nne asubuhi,na badae kutakuwa na dua nyumbani tabata pamoja na chakula cha mchana kwa watakaojaliwa naomba tuungane pamoja kwenye dua hii,asanteni nawapenda wote

No comments:

Post a Comment