Saturday, August 23, 2014

WAJUE WADADA WATATU WANAOKIMBIZA SOKO LA FILAMU KWA SASA


Mcheza filamu za kitanzania Wastara Juma Issa ametajwa kuwa tishio kwa hivi sasa kwenye filamu za bongo baada ya kuonesha uwezo wake mkubwa wa kucheza kila kipande anachopewa toafuti na wenzake,na ndio msanii mkongwe anaeongoza kwa kucheza filamu nyingi za kushirikishwa kwa mwaka huu kuliko mrembo yoyote wa tasnia hiyo

Mbali na filamu yake ya Last Decision kufanya vizuri sokoni na kuwapa kiwewe wasanii wenzake kwa namna alivyofanya uzinduzi wake mitaani Wastara pia anatajwa kama msanii pekee anaeongoza kwa kuvaa mavazi ya heshima kuliko msanii yoyote bongo

Hizi ni baadhi ya filamu ambazo ameonesha uwezo mkubwa kwa mwaka huu mpaka sasa ni Gumzo,Kijacho,Njia Panda,Faulo,Last Decion ya kwake na Uminifu dhaifu inayotoka hivi karibuni pia filamu ya Ughaibuni amabayo ipo mbioni kutoka amabayo amechezea London


Huyu jina lake maarufu ni Odama amejipatia umahaarufu mkubwa kwa filamu zake nzuri zenye mafundisho na ndio anashikilia nafasi ya pili kwa hivi sasa kwenye tasnia ya filamu bongo mpaka sasa ametoa filamu nyingi za kusisimua na kwa hivi sasa anatamba na filamu yake ya In side,na jicho langu

Salma Jabu nisha anatajwa kuwa namba tatu na ndio msanii amabae ameweza kuliteka soko la filamu kawa mda mfupi kutokana na juhudi zake mpaka sasa anatamba na filamu yake ya zena na betina,gumzo,tikisa pamoja na pusi na paku

No comments:

Post a Comment