Friday, July 25, 2014

PATI YA KAJALA YAIBUA MAMBO NCHINI CHINA

Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ameangusha pati nchini China kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na kuibua minong’ono juu ya chanzo cha jeuri hiyo ya fedha.
Kufuru hiyo ya fedha ilianzia jijini Dar katika bethidei ya mwanaye (Paula) hivi karibuni ambapo awali alikwenda kutoa misaada ya vitu mbalimbali katika Shule ya Sinza Maalum kisha kuangusha bonge la sherehe katika Hoteli ya Sea Cliff.
Baada ya vurugu hizo ambazo kimsingi zilidaiwa kuteketeza milioni kadhaa, siku chache baadaye (Julai 22, mwaka huu), kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, Kajala alitupia picha za sherehe yake ya kuzaliwa aliyoifanyia nchini China katika Mgahawa wa Waitaly uliyopo Guahnzu.


 Chanzo kilichokuwepo katika sherehe hiyo kilisema, Kajala aliwaalika marafiki zake kibao wa nchini humo akiwemo mpenzi wake wa zamani, Petty Man ambapo walikula na kunywa kwa bili yake kitu ambacho wengi walihoji kuhusiana na alikozipata fedha hizo.

No comments:

Post a Comment