Wednesday, July 23, 2014

BABY MADAHA, SHILOLE WATIFUANA

MTIFUANO mzito umeibuka kati ya mastaa wa Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na Baby Madaha baada ya kurushiana vijembe.

Baby Madaha alinukuliwa akisema kuwa Mwezi wa Ramadhani unambana kiuchumi, kwa vile kumbi nying za starehe zimefungwa, hivyo anakosa shoo na Shilole alisema anamshangaa Madaha kwa kukosa hofu ya Mungu, huku akimchana kuwa, haweki akiba, anaishi maisha ya kutegemea shoo ndiyo maana anaulalamikia mwezi huu.






Madaha alivyoelezwa kuhusu maoni ya Shilole, alikuja juu na kutema cheche: “Shilole anatafuta kiki kupitia jina langu, kwanza si hadhi yangu. Siwezi kujibishana na msanii anayetegemea shoo za kwenye vigodoro, akatafute pa kutokea.”

No comments:

Post a Comment