Saturday, April 05, 2014

DUDE AKIRI KUBEBESHWA MADAWA YA KULEVYA

STAA wa filamu za Kibongo , Kulwa Kikumba
‘Dude’ amekiri kubebeshwa madawa ya
kulevya bila kujua na kujikuta akiponea
chupuchupu kutokana na umaarufu wake .

Akizungumza na paparazi wetu , Dude
alisema amewahi kubebeshwa unga na
rafiki yake wa karibu ambaye hakumtaja
jina na walikuwa wakitokea Nairobi nchini
Kenya kuja Tanzania. Alisema wakati
wanaanza safari alipewa koti la baridi na
rafiki yake huyo , akalivaa kumbe ndani yake
lilikuwa limeshonewa pakti za unga .
Walisafiri kwa gari na kila walipokutana na
polisi wanaokagua hawakumkagua Dude
kwani waliishia kupiga naye picha na
kumsifia kwa kazi yake mpaka alipofika jijini
Dar es Salaam .
“ Kila tulipokuwa tunakutana na polisi rafiki
yangu alikuwa akiwawahi na kuwaambia
kwamba yupo na mimi ambapo walifurahia
kuniona na kupiga picha na mimi bila
kunikagua chochote , ” alisema
Dude.
Baada ya kupita vizingiti vyote, waliingia
jijini Dar es Salaam maeneo ya Kinondoni
Manyanya alipokuwa akiishi rafiki yake huyo
ambapo alimwambia avue koti, akaanza
kufungua mzigo aliokuwa ameushonea kwa
ndani.
Dude alijikuta akishikwa na tumbo la kuhara
kutokana na mshtuko alioupata baada ya
kuona rafiki yake huyo akitoa madawa ya
kulevya .
“ Jamaa alinipa shilingi elfu hamsini za Kenya
na ni baada ya kufika Dar ndipo niligundua
kwamba nilikuwa nimebebeshwa unga lakini
yule jamaa alishakamatwa na anatumikia
kifungo nchini Pakistani , ” alisema Dude.
Hata hivyo Dude aliwashauri mastaa
wenzake kuwa makini na marafiki zao kwani
siyo wote wanaokamatwa wamebeba unga
kwa kujua bali wengine wanabebeshwa tu
bila kujua

No comments:

Post a Comment