Monday, February 03, 2014

KUMBE MZUNGU WA SHILOLE NI MWANAUME TATA

Yeleuuuwi! Siku chache baada ya msanii wa
sinema na muziki Bongo, Zuwena Mohamed
‘Shilole ’ kujinadi na mchumba wa Kizungu
aliyejulikana kwa jina moja la Ankar , siri
imefichuka kwamba jamaa huyo ni
mwanaume tata .

Kikizungumza na Ijumaa Wikienda kutoka
London, Uingereza, wikiendi iliyopita , chanzo
hicho makini kilisema mwanaume ambaye
hivi karibuni Shilole alijinadi kuwa ni
bwana ’ ke siyo kwani huko London baadhi
ya watu wanamfahamu kama mwanaume
tata kijinsia.

“ Yule jamaa anapenda sana kukaa na
wanawake, sijawahi kumuona na wanaume
wenzake , kazi kukata tu mauno na
wanawake. Nilishangaa sana Shilole kusema
eti ni mchumba ’ ke wakati hapa London
(Uingereza) ni maarufu sana kwa kushiriki
pati za wanawake.
WAPENZI: Zuwena Mohamed ‘ Shilole’
akiwa na ' mchumba wake', Ankar .
“ Maskini Shilole , pale imekula kwake ,
hakuna chochote , ” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kunyetishiwa habari hizo , gazeti
hili lilimtafuta Shilole ambapo alikuwa na
haya kusema :

“ Jamani imeniuma sana kwani nilikuwa sijui ,
nimeligundua hilo baada ya kuambiwa na
watu , nilipigiwa simu kutoka Uingereza
kwamba yule mwanaume siyo hivyo sina
mpango naye tena kwa kweli, ” alisema
Shilole anayetamba na kideo cha Nakomaa
na Jiji

GP

No comments:

Post a Comment