Thursday, January 02, 2014

Sijaona staa wa kumfananisha na mwanangu:mama Kanumba

MAMA KANUMBA: SIJAONA STAA WA KUMFANANISHA NA MWANANGU

MAMA wa msanii aliyekuwa nguli wa filamu nchini marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa  amenyanyua kinywa chake na kutema cheche kuwa katika mastaa wote wa filamu Bongo, hajaona hata mmoja wa kumfananisha na mwanaye kimuonekano na hata katika uigizaji wake.

Akipiga stori na Centre Spread mama Kanumba alisema hayo kutokana na mastaa wengi kutamani awape nafasi ya kucheza kama Kanumba katika filamu yake anayoiandaa inayohusu maisha ya mwanaye tangu utotoni, na kudai katika wote hajaona mwenye kigezo cha kumpa nafasi hiyo.

“Siyo kwamba hawana kiwango kizuri cha kumfikia mwanangu, isipokuwa kwa mtazamo wangu naona nikimshirikisha staa yoyote katika kipengele hicho nitakuwa nimevurunda kazi yangu…nitaandaa tamasha maalumu la kumsaka kijana anayefanana na Kanumba,” alisema mama huyo.

GP

No comments:

Post a Comment