STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka amejifungua mtoto wa kike kwa njia ya upasuaji mwanzoni mwa wiki hii katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliyopo jijini Dar.
Rose Ndauka alisema anamshukuru sana Mungu kwa kumjaalia kujifungua salama huku mwanaye huyo akiwa na afya njema.
“Ki ukweli kabisa namshukuru sana Mungu kwa zawadi ya mtoto kwa maana nimejifungua salama kabisa,mimi na mtoto tuko vizuri na nafurahi sana kuingia kwenye ulimwengu mwingine kabisa wa cheo kipya cha kuitwa mama,” alisema Rose.
Akasema hivi sasa ataweka shughuli zote pembeni kwa ajili ya kuanza kumlea mtoto mpaka atakapofisha umri ambao anastahili kuachwa ndipo ataendelea na shughuli zake za sanaa.
No comments:
Post a Comment