Mwanadada Jacqueline Dustan ambaye ni msanii wa filamu aliyeibukia kwenye Shindano la Maisha Plus season II, ameonekana kung’ang’ania kuzaa na Mzungu kufuatia maelezo yake kwamba harudi Bongo mpaka atundikwe mimba na mtasha.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu akiwa nchini Thailand, Jack alisema uwepo wake nchini humo kwa muda mrefu anajilengesha kwa mwanaume wa Kizungu ambaye atampenda na ikiwezekana amzalie mtoto.
“Kwa kweli nitarudi Bongo endapo tu nitapata mtoto mmoja wa kitasha, sasa niko bize kutafuta mchumba ambaye ni salama kwangu ili niweze kupata naye mtoto mmoja tu,” alisema Jack.
Ni takriban mwezi wa sita sasa msanii huyo yuko nchini humo huku anachokifanya kikiwa hakijulikani licha ya kuwepo kwa madai kuwa, wasanii wengi wanaokwenda huko wanajiuza
GP
No comments:
Post a Comment