Thursday, January 09, 2014

Agnes Masogange:sina tabia ya kutembea na mume wa mtu


VIDEO Queen mwenye figa matata Bongo, Agnes Jerald ‘Masogange’ amesema anaogopa kama ukoma kutembea na mume wa mtu kama wafanyavyo baadhi ya watu.

Akizungumza na paparazi wetu, Agnes ambaye hivi sasa amejiingiza kwenye soko la filamu, alisema anaogopa sana kuingia kwenye uhusiano na mume wa mtu ndiyo maana anaona bora aendelee na mpenzi wake wa siku zote kuepuka uhasama.

“Sina tabia ya kushobokea kabisa waume za watu,  bora niendelee na mtu wangu wa siku zote na kama tukishindwana basi bora nitafute mwingine lakini awe wangu peke yangu,” alisema Masogange.

GPL

No comments:

Post a Comment