Msanii wa filamu, Steve Nyerere amesema Wema Sepetu alikuwa
hajitoi kwenye matatazo ya wasanii wenzake wa filamu na ndio maana
wasanii wengi wa filamu wakashindwa kuhudhuria katika mazishi ya baba
yake, Balozi Isaac Abraham Sepetu mwishoni mwa mwezi uliopita.
Akizungumza leo Steve,amesema anawataka watu waache kumtupia lawama Vicent Kigosi aka ‘Ray’ wakati mwanadada huyo alikuwa hahudhurii katika matatizo ya wenzake.
“Mnamlaumu bure Ray jambo ambalo hajafanya kwakuwa Ray ni jalala
basi kila kitu mnamtupia,jamani mwacheni apumzike,” amesema Steve.
“Sisi katika Bongo Movie Unity tuna uongozi, tuna
mwenyekiti,tuna mwenyekiti wa mipango ambaye ndio mimi, na tuna makamu
wa mwenyekiti ambaye ndio mimi na tuna makamu mwenyekiti ambaye ni Irene
Uwoya. Lakini sisi taratibu zetu kwenye misiba kama unaona kwenye
misiba yetu tunajitoa,lakini linavyotufika tunaangalia ni mwanachama
gani naye anakua anajitoa katika misiba ya wenzake
habari kwa hisani ya bongo movie
No comments:
Post a Comment