Wednesday, September 28, 2016

WASTARA APATA MTONYO WA SHILINGI MILIONI 400 KWA MWAKA





Kupitia ukurasa wake wa instagram wastara ameandika maelezo haya na kuweka picha hizi


leo tal 28 nimesain rasmi mkataba wa kuwa balozi wa company ya uuzaji wa sim ya china KZG
kuanzia leo mim wastara juma issa nimeanza rasmi kazi ya ubalozi wa KZG itakayoningizia milion 400 kwa mwaka
kikubwa ni kuni support kwa kila hatu naimani ndani ya mafanikio yangu nyuma yake kuna watanzania wenzangu wengi watakao nufaika na kujipatia vibarua kupitia wastara
asanteni kwa ushirikiano kwa wale wote walihudhuria tukio hili.....

Wednesday, September 21, 2016

KALAMBATI LOBO YA JB KUONESHWA SIBUKA MAISHA IJUMAA KABLA YA KUINGIA SOKONI


 ⁠⁠⁠Mcheza filamu maarufu Jacob stephen (JB) amefanya mkutano na waandishi wa habari kwa lengo la kutambulisha mfumo mpya wa kuonesha filamu kupitia media ya Sibuka Maisha channel 111 kwenye startimes kabla ya kuingia madukani.
Amesema filamu hiyo inaoneshwa kwa mara ya kwanza Ijumaa tarehe 23 mwezi huu saa 3 usiku na kurudiwa Jumamosi na Jumapili ili kuwapa muda mashabiki zake waweze kuona filamu hiyo
Aidha ameishukuru kampuni ya Steps entertainment kwa kuanzisha mfumo huu mpyaa wa kuonesha filamu kabla hazijaingia sokoni
Filamu hii inatarajia kuingia sokoni Jumatatu 26 mwezi wa 9 nchi nzima,kwa sasa hivi Jb anatamba sokoni na filamu ya chungu cha tatu akiwa na Wema Sepetu na wasanii wengine wengi.

Thursday, June 02, 2016

KAJALA MASANJA KUJA NA SIKITU BAADA YA MWEZI WA RAMADHANI





Mcheza filamu mwenye jina kubwa Tanzania Kajala Masanja anatarajia kuachia filamu yake ya Sikitu baada ya mwezi mtukufu wa ramadhani,

akifunguka kiafrika bila hofu yoyote amesema kwenye filamu huyo amecheza na wasanii mbali mbali akiwemo mzee Majuto na Hemed Suleiman itakuwa funzo kwa wanandoa wanaoishi na wadogo zao wa kike

Kjala amesema filamu hiyo inasambazwa na kampuni kubwa ya usambazaji nchini steps entertainment

NEEMA NDEPANYA KUJA NA KOBE LA MCHANA MWEZI HUU

FILAMU YA ANGELA KUTOKA KWA ROSE NDAUKA HII HAPA

Wednesday, June 01, 2016

BAADA YA CHURA KUPIGWA PINI SASA SNURA ANAWALETEA MENDE

 Ikiwa imepita wiki kadhaa tangu wimbo wa Snura mrembo kutoka kiwanda cha burudani bongo kufungiwa ameamua kuja na wimbo mwingine unaitwa Mende,

Snura amesema wimbo wa mende anafikilia kuutoa baada ya mwezi mtukufu wa ramadhani unaotarajia kuanzi mwanzoni mwa mwezi huu
 "wimbo wangu wa chura umefungiwa sasa hivi nakuja na wimbo unaitwa mende nimepanga kuutoa baada ya ramadhani
wimbo wa chura umefungiwa baada ya serikali kuona auna maadili ya kitanzania kutokana na jinsi wimbo huo uluvyoimbwa na video ya wimbo huo kudhihilisha kuwa wimbo auna maadili